Mama ahukumiwa jela kwa kumlazimisha binti yake kuolewa.

Mama mwenye umri wa miaka 40 Sakina Muhammad Jan raia wa Australia amekuwa mtu wa kwanza kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kukutwa na hatia ya kumshurutisha binti yake mwenye umri wa miaka 21 kuolewa na mwanaume ambaye baadae alimuua.
Mwanamama huyo alipatikana na hatia ya kumlazimisha Ruqia Haidari kuolewa na Mohammad Ali Halimi mwenye umri wa miaka 26 mwaka 2019 baada ya kubadilishana kiasi cha fedha na mwanaume huyo aliyemuoa binti yake.
Wiki sita baada ya harusi Halimi alimuua mke wake wake na alipatikana na hatia ambayo ilisababisha kuhukumiwa  kifungo cha maisha jela.
Siku ya Jumatatu Bi Sakina Jan ambaye alikana hatia  alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kile hakimu alichokiita “Shinikizo lisilovumilika” aliloweka kwa binti yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *