“Real Madrid ndio klabu kubwa zaidi duniani” – Mama Mbappe

Siku moja baada ya mwanae kutambulishwa rasmi kwenye klabu ya Real Madrid, Mama yake Kylian Mbappe, Fayza Lamari, amesema Real Madrid ndio klabu kubwa zaidi duniani.

Nahodha huyo wa Ufaransa alitambulishwa rasmi na wababe hao wa Uhispania siku ya Jumanne baada ya kuondoka Paris Saint-Germain kama mchezaji huru.

Kwa mujibu wa Fayza, tofauti kati ya klabu hizo mbili iko wazi mnoo.

“Real Madrid ndio klabu kubwa zaidi duniani,” alisema Fayza .

“Siku ya Jumanne nilihisi utofauti,…..Parc des Princes (PSG) ni klabu nzuri sana, Lakini ukifika Real Madrid, unahisi uzito wa taasisi.”

Ukiacha kuwa mama mzazi, Fayza pia anafanya kazi kama wakala wa Mbappe.

Kwa upande wa Baba, Wilfrid Mbappé, yeye ni kocha wa soka huku mdogo wake aitwae Ethan, ni mchezaji anayekipiga na klabu ya Lille ya nchini Ufaransa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *