SIMBA WARUDI NA MIL 600 TZ KUMPATA MPANZU

INAELEZWA kuwa Mabosi wa Simba wamerudi tena kwa mara nyingine wakifosi zaidi kuinasa ya mchezaji wa AS Vita Elie Mpanzu.

Simba hadi jana walikuwa wametuma ofa ya dola 200,000 sawa na Tsh Milioni 540, wakati huo AS Vita walikuwa wanahitaji Dola 250,000.

Asubuhi ya Leo Simba wameongeza tena mzigo hadi kufikia dola 225,000 sawa na Tsh Milioni 607, safari hii Simba wako siriazi zaidi wanahitaji saini ya Mpanzu kuliko kitu chochote.

Wakala wa mchezaji huyo alipotafutwa kuzungumzia ukweli wa dili la Mpanzu na Simba kama liko wazi hakutoa jibu la moja kwa moja.

“Siwezi kusema kama dili ni wazi au vipi, lakini Mpanzu anahitajika na timu nyingi za Afrika lakini mimi ni marafiki zangu Simba” Wkala wa Mpanzu Papido

Baada ya Kibu Denis kutorokea Norway sasa Simba wamerudi kwa kasi kubwa kukamilisha usajili wa Mpanzu ambao awali ni kama dili lilikuwa limekufa.

Inaelezwa kwamba dili hilo likikamilika miongoni mwa wachezaji ambao wanapewa nafasi kubwa ya kutolewa ni Fredy Michale Koublan, kwa sababu Kocha wa timu hiyo haridhishwi na kiwango chake.

Awala wakala wa Mpanzu alizungumzia namna ambavyo ni ngumu kufanya biashara na Simba haswa kipindi cha usajili kama hivi sasa.

“Tofauti ya Simba na Yanga ni kuwa Yanga wanapotaka Mchezaji unawasiliana na Mtu mmoja tu ila Simba watu ni wengi sana kwa dili moja, mara Salim, mara Mulamu mara Magori.”

“Pia walikuja kwa kuchelewa sana kuhusu kumtaka Mchezaji wangu Ellie Mpanzu, hata hivyo hawezi kwenda Simba anaenda Ulaya, lakini nilishawaambia Simba ipo siku watanitafuta, nitawapa Wachezaji wakishanilipa pesa yangu dola 5,000 kuna dili tulifanya na wanajua” Alisema Papida wakala wa Ellie Mpanzu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *