
Waandamanaji wavamia gereza na kuwaachilia mamia ya wafungwa
Waandamanaji nchini Bangladesh wamevamia gereza siku ya Ijumaa na kuwaachilia “mamia” ya wafungwa kabla ya kulichoma moto gereza hilo, afisa wa polisi ameliambia shirika la habari la AFP. “Wafungwa wametoroka gereza na waandamanaji wamechoma moto gereza”, afisa wa polisi amesema, akizungumza kwa sharti la kutotajwa. “Sijui idadi ya wafungwa waliotoroka lakini itakuwa mamia,” ameongeza….