Trent Alexander Arnold kuinunua FC Nantes ya ligi kuu Ufaransa.

Beki wa kulia wa  klabu ya Liverpool Trent Alexander-Arnold mwenye umri wa miaka 25 ametuma ofa ya kuinunua klabu ya FC Nantes inayoshiriki ligi kuu Nchini Ufaransa Ligue 1 kupitia kampuni ya uwekezaji yenye makao yake Jijini London.

Taarifa kutoka Nchini Ufaransa zinaeleza kuwa ofa aliyoweka mchezaji huyo inaripotiwa kufikia €100m sawa na  Bilioni 302.9 za Kitanzania pamoja na nyongeza ya €40m sawa na  Bilioni 121 za Kitanzania.

 

Mazungumzo kati ya mmiliki wa sasa wa klabu hiyo Waldemar Kita yalifanyika siku ya jana kwa mara ya tatu na baba mzazi wa nyota huyo wa Liverpool Micheal Anorld huku dili hilo likionekana kuwa gumu kukamilika.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *