Zanzibar Finest kumrithi mzungu Mamelodi.

feitoto

Taarifa kutoka Afrika Kusini zimeripoti kuwa klabu ya Mamelodi Sundowns inajiandaa kutuma ofa ya pili kwa klabu ya Azam kwa ajili ya kupata huduma ya kiungo Feisal Salum ili kuziba pengo la Bongani Zungu na Gaston Sirino ambao walitangaza kuachana nao hivi karibuni.

The brazilians wameamua kuwa serious na dili hilo baada ya kutuma ofa kubwa zaidi ya Rand milioni 32 (TZS bilioni 4.7) kutokana na ile ya  kwanza ya Rand milioni 25 (TZS bilipni 3.7) kupigwa chini na Azam FC.

Taarifa zinaeleza kuwa Matajiri wa Jiji la Dar es Salaam Azam FC wanahitaji Rand milioni 36 (TZS bilioni 5.2) ili kumuachia mchezaji huyo nyota wa Timu ya Taifa ya Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *