50 CENT Afichua siri ya utofauti wa kufanya series na single movie.

Mwigizaji na mtayarishaji wa filamu kutoka nchini Marekani anayefahamika zaidi kama 50 Cent amefunguka kwanini kutengeneza tv series ni bora kuliko kuandaa movie ya fupi ya kawaida.

 

Kupitia mahojiano aliyoyafanya msanii huyo maarufu ambaye pia ni rapa amesema kufanya series haihitaji msanii maarufu inahitaji kipaji pekee ila kufanya movie inahitaji msanii maarufu .

 

50 Cent amefanya zaidi ya Series 13 zilizomtambulisha kwenye sanaa ya uigizaji huku za hivi karibuni ikiwa ni iliyotoka mwaka 2021 inayojulikana kama Hip Hop Uncovered, mwaka 2023 Expend4bles na mwaka huu Boneyard.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *