Amuua Jirani aliyemuuliza Kwanini Hajaoa na Ana Miaka 45

Mwanamume mwenye umri wa miaka 45 nchini Indonesia anadaiwa kumpiga jirani yake mwenye umri wa miaka 60 hadi kufa baada ya kukasirishwa na ung’ang’anizi wa jamaa huyo wa kumuuliza kwa nini bado alikuwa mseja.

 

Inasemekana mshtakiwa alienda nyumbani kwa jirani yake akiwa amebeba kipande cha mbao na kuanza kumshambulia mwathiriwa bila tahadhari.

 

Akihojiwa na polisi, alisema alikuwa amedhamiria kumuua jirani yake kwa sababu aliumizwa na jinsi mara kwa mara alivyokuwa akimuuliza kwa mzaha kwanini hajaoa mpaka leo.

📸 : South Tapanuli Regency Police

#Indonesia

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *