Muuaji wa Wanawake Sita Pamoja na Mkewe, Atoroka Jela

muuaji kenya

Collins Khalusha Mtuhumiwa wa mauaji ya wanawake Sita akiwemo na mkewe wa ndoa, ambapo anadaiwa baada ya kutekeleza mauaji hayo aliitupa miili ya wanawake hao katika machimbo ya Kware katika kaunti ya Embakasi, ametoroka asubuhi leo Jumanne Agosti 20, 2024 kwenye kituo cha polisi cha Giriri, Nairobi Kenya

Katika kesi yake Mtuhumiwa huyo ambaye alikiri kuhusika na mauaji hayo na alikuwa miongoni mwa watuhumiwa 13 waliotoroka kituoni hapo.

Kamanda wa Polisi Nairobi, Adamson Bungei akizungumza na Gazeti la Daily Nation amesema msako umeanza ili kuwakamata tena waliotoroka.
“Tunafuatilia suala hili kwa ajili ya hatua zaidi,” amesema.

Maofisa hao wamesema walienda katika vyumba vya watuhumiwa hao kwa ajili ya kuwapatia kifungua kinywa ndipo walipogundua walikuwa wametoroka.

Wamesema walipofungua mlango wa selo, walishtuka baada ya kubaini watuhumiwa 13 walitoroka kwa kukata matundu ya nyaya kwenye dirisha.

Khalusha alikuwa akisubiri kufikishwa mahakamani kwa ajili ya kujibu mashtaka yake siku ya Ijumaa, Agosti 23, 2024.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *