AHADI 5 ZA RAIS SAMIA KWA WAHITIMU WA DARASA LA SABA

Rais Samia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, ametoa ahadi tano kwa wanafunzi 1,230,780 wanaofanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi unaomalizika leo nchini, huku akisema ni zawadi kwao ambayo serikali inahakikisha inatimia.

Katika taarifa aliyoiandika kwenye WhatsApp Channel, Rais Samia alisema anawatakia kila la heri wanafunzi wa darasa la saba watakaomaliza elimu ya msingi leo.

“Mnatoka katika hatua moja ya elimu na malezi kwenda nyingine katika safari yenu ya kujiandaa kutoa mchango wenu wa maendeleo kwa taifa letu. Serikali imeandaa mazingira sahihi ili kufikia lengo,”alisema.

Alisema ahadi yake kwa wanafunzi hao katika safari ya elimu na maisha ambayo tayari inatekelezwa uhakika wa kupata nafasi ya kujiunga kidato cha kwanza 2025 kwa kila atakayefaulu.

Nyingine ni miaka minne ya sekondari ya awali bila ada; miaka miwili ya kidato cha tano na sita bila ada; chuo cha ufundi katika kila wilaya kwa watakaochagua njia hiyo; na mikopo ya elimu ya juu kwa watakaofaulu kwenda vyuo vikuu.

Alisema ahadi hizo zinakwenda sambamba na kuendelea kuboresha sera za uchumi, ili kuzalisha fursa zaidi kwa kila mmoja kadiri wanavyoendelea kukua na kuingia katika nguvu kazi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *