Asake wa Nigeria aweka rekodi Billboard.

Rapa wa Nigeria Ahmed Ololade maarufu kama Asake ameweka rekodi ya kuingiza nyimbo 50 kwenye chati ya Billboard U.S. Afrobeats Songs, akiwa ni msanii wa kwanza kutoka Afrika kufanya hivyo kwenye historia ya chati hiyo.

Msanii huyo ambaye nyimbo zakie zimekuwa zikiwavutia watu wengi duniani kutokana na mchanganyiko wa kipekee wa midundo ya Afrobeat, amapiano na melody za kuvutia umeonekana kuliteka zaidi soko la muziki Nchini Marekani na kupata wasikilizaji wengi.

Wasanii wa Nigeria wamekuwa wakifanya vizuri kwenye kwenye chati za Billboard U.S kwenye muziki wa Afrobeats na mara kadhaa baadhi ya ngoma zao zimekuwa zikiongoza chat hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *