Azam kumaliza kambi ya Pre-Season Morocco na Wydad ya Rulani Mokwena

Klabu ya Azam leo usiku itahitimisha kambi ya maandalizi ya msimu iliyoweka kwa wiki kadhaa huko Benslimane Morocco kwa mchezo mkubwa wa kirafiki dhidi ya Wydad AC ambayo ni moja ya klabu kubwa nchini humo na barani Afrika kwa ujumla.

 

Mchezo huo dhidi ya Wydad ambao wanafundishwa na aliyekuwa kocha wa Mamelodi Sundwons Rulani Mokwena utachezwa majira ya saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

 

Picha juu ni kocha Mokwena akikabidhiwa jezi ya Azam Fc na mmoja wa watumishi wa idara ya masoko wa Azam @mkisi_azam wakati alipokuja na Mamelodi kwenye mechi za ligi ya Mabingwa msimu uliopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *