Bahati Bukuku Afunguka Juu ya Uwoya Kuokoka

Mwimbaji mkongwe wa muziki wa Injili Bongo, Bahati Bukuku amefunguka kuhusu Irene Uwoya kuokoka na kuwa Mchungaji.

“Kitendo cha Irene Uwoya kuokoka na kuamua kuwa Mchungaji ni kitendo cha Kimungu zaidi watu wasichukulie poa. Sio rahisi mtu kama Irene Uwoya kuamua kubadilika na kumrudia Mungu, kwa ufahari wake angeweza hata kufanya maovu mengine ya dunia na watu wangemshangilia, lakini ameamua kuokoka na kumrudia Mungu”

 

“Kwanza ni mrembo, ni staa, ana pesa, ana muonekano mzuri, warembo kama yeye ni ngumu kuona wanaokoka. Nashindwa kuelewa wanaomsema vibaya walitaka awe nani haswaa ndio waone amebadilika? kwasababu alipokuwa kwenye maovu bado walimsema vibaya wakimtaka amrudie Mungu, haya amerudi kwa Mungu bado watu haohao wanasema hafai kuwa Mchungaji bora abaki kwenye upagani”

 

“Piga kazi Irene, unapoamua kufanya kazi ya Mungu lazima ujiandae kwasababu huku kuna maadui wengi, shetani hayupo tayari kukupoteza kwasababu anajua ukiondoka kwenda kwa Mungu lazima utaondoka na wafwasi wake kutokana na jina lako”- Pastor Bahati Bukuku.

 

Imeandikwa na @georgechikao_

#bambadigital

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *