Benchikha awavuta wachezaji na makocha Simba Aljeria

Baada ya aliyekuwa kiungo wa klabu ya Simba, Babacar Sarr kutangazwa kama mchezaji mpya wa klabu ya JS Kabylie ya Algeria kama mchezaji huru baada ya kumalizana na Wekundu hao wa Msimbazi mpaka sasa klabu ya JS Kabylie ina wachezaji na watumishi wa bechi la Ufundi zaidi ya watano kutoka Simba.

 

Babacar raia wa Senegal anaungana na aliyekuwa kocha wa Simba Sc, Abdelhak Benchikha pamoja aliyekuwa kiungo wa Simba Sc, Sadio Kanoute bila kusahau makocha wasaidizi wa Benchikha Simba kama kocha wa makipa na viungo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *