Dangote Pamoja na Utajiri wake wote, Anaishi Kwenye Nyumba ya Kupanga

dangote anaishi nyumba ya kupanga

Inawezekana wengi wetu tunajitazama kwenye mafanikio pale tunapo miliki nyumba zenye hadhi na muonekano mzuri.

Hii imekuwa tofauti kwa Tajiri namba moja barani Afrika, Aliko Dangote ambaye amewashangaza wengi na kuzua mijadala katika vijiwe vya kidijitali baada ya kusema hana nyumba nchi nyingine yoyote zaidi ya Nigeria.

“Sababu ya kutokuwa na nyumba London au Marekani ni kuwa nilitaka kuangazia ukuaji wa viwanda nchini Nigeria,”.

“Ikiwa nitakuwa na nyumba kote Marekani na kwingineko, singeweza kutuliza akili na kufanya kitu kwa ajili ya watu wangu.” alisema Dangote.

Dangote aliorodheshwa kwenye jarida la Forbes mwezi Januari kama mtu tajiri zaidi barani Afrika kwa kipindi cha miaka 13 mfululizo, licha ya matatizo ya kiuchumi yanayoikumba nchi yake.

Huku Utajiri wake ukipanda kwa $400m zaidi mwaka jana, na kumpa thamani ya jumla ya $13.9bn (£10.7bn), Forbes walisema wakati huo.

Na Matajiri wengine wa kiafrika wanamiliki majumba kwenye miji mikubwa duniani kama vile London, Dubai, Washington na Paris, lakini kwake imekuwa tofauti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *