Figo ya kaka yake aliyopandikiziwa Director TG Omori imefeli tena.

Muongozaji wa video za muziki nchini Nigeria ThankGod Omori maarufu TG Omori amefunguka kuwa hali yake ya kiafya ni mbaya kutokana na figo aliyochangiwa na kaka yake ili kunusuru maisha yake kufeli kwa mara nyingine.

Omori aliweka wazi kupitia  ukurasa wake wa Instagram kuwa kaka yake wa pekee amemchangia moja ya figo yake ili aweze kuokoa maisha yake akichapisha picha yake akiwa amelazwa hospitalini huku anapumua kwa kutumia mashine ya oksijeni.

Omori ambaye amekuwa nje ya tasnia ya muziki kwa muda mrefu kutokana na hali yake ya kiafya amekuwa akitoa taarifa kuhusu matatizo yake ya afya kupitia mitandao yake ya kijamii huku leo akizua taharuki kwa mashabiki zake baada ya kuweka wazi kuwa upandikizaji wa Figo aliochangikiwa na kaka yake umeshindikana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *