Kamala Harris amchagua Tim Walz kuwa mgombea mwenza wake

Kamala Harris amemchagua gavana wa Minnesota Tim Walz, kuwa mgombea mwenza wake katika uchaguzi wa rais wa Marekani, vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti.

Bi Harris na mgombea mwenza wake wanatarajiwa kuanza ziara ya kampeni katika majimbo yanayosadikiwa kuwa na ushindani mkali, mkutano wa kwanza ukipangwa kufanyika huko Philadelphia baadaye leo.

Kura ya maoni ya hivi punde ya kituo cha CBS, mshirika wa BBC wa Marekani, inawaonyesha Bi Harris na Trump wakiwa katika kinyang’anyiro kikali kitaifa, huku Mgombea huyo wa chama cha Democratic akiongoza kwa pointi moja dhidi ya mpinzani wake wa chama cha Republican Donald Trump.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *