Kenya kumechafuka…! maandamano yarejea tena kwa mara nyingine.

Maafisa wa Polisi nchini Kenya wameingia katika mitaa mbalimbali ili kukabiliana na mamia ya waandamanaji katikati mwa miji mikubwa Nchini humo ikiwemo Nairobi na Mombasa.

Waandamanaji hao wamedai lengo la maandamano hayo ni kutaka mageuzi yafanyike katika mfumo wa usimamizi wa rasilimali za umma, na kudai haki kwa wenzao waliouawa wakati wa maandamano yaliyopita na baada ya maandamano.

Ikumbukwe, hivi karibuni iliokotwa miili tisa ya watu iliyofungwa kwenye mifuko katika bonde lililopo karibu na kituo cha polisi Kware jambo lililozua taharuki kubwa kwa baadhi ya watu.

Licha ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini humo kujitokeza na kuweka wazi kuwa polisi hawahusiki na mauaji hayo huku mshukiwa wa mauaji hayo akiwa mikononi mwa polisi bado raia wamepoteza imani kwa jeshi hilo pamoja na viongozi wa Nchi yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *