Klabu ya Simba leo Julai 23,2024 imetoa taarifa kuwa Mchezaji wake, Kibu Denis Prosper hajaripoti kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa mwaka 2024/2025.
“Tunapenda kuutarifu umma kuwa Simba tulimuongezea Kibu mkataba wa miaka miwili zaidi utakaoishia June 2026 na kumlipa stahiki zake zote za kimkataba, hata hivyo Mchezaji huyu amekuwa akitoa sababu kadhaa wa kadhaa zinazomfanya kushindwa kuripoti kambini”
“kutokana na utovu huu wa kinidhamu klabu itamchukulia hatua stahiki za kinidhamu na umma utapewa taarifa”