Mafuriko yalizoa kasri la Drake huko Toronto, Canada

Majanga ya mafuriko usifikiri ni Tanzania tu, hata huko mbele kwa wenzetu mtindo ni ule ule, na safari hii Rapa maarufu duniani, Drake yamemfika baada ya jumba lake la kifahari (kasri) lililopo nchini Canada kusombwa na mafuriko.

Drake alichapisha video ya jumba lake lililofurika maji kwenye ukurasa wake wa instagram.

Jiji la Toronto lilikumbwa na dhoruba kali iliyosababisha mafuriko na kukatika kwa umeme siku ya Jumanne.

Mtu ambaye hakutambulika anaonekana kwenye video hiyo akisukuma milango ya vioo huku maji yakiingia ndani kwa kasi kwenye chumba hadi chumba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *