Muna Love Ajifungua Mtoto Mwingine wa Kiume.

Muna Love amechapisha picha kwenye ukurasa wake wa instagram akiwa na mtoto wake mchanga kwenye moja ya Hospitali nchini Canada na kuambatanisha na andiko lililowagusa wengi huku akimshukuru Mungu kwa kumpatia mtoto mwingine na kumkabidhi mikononi mwa Yesu akiahidi kuwa mtoto huyo atatumika kulitangaza jina la Yesu pamoja na mama yake.

Msanii huyo kupitia waraka huo amemshukuru marehemu mwanae Patrick kwa kumsaidia kumjua Yesu na kumuomba radhi kwa kumlaumu kumuacha mapema huku akitangaza kumpata mtoto wa kiume aliyempa jina la “Testimony” akisema atampatia pia jina lingine la Kiislamu ambalo atalitaja baadae ili mtoto huyo atumike kumtangaza Mungu katika dini zote.

“PATRICK naimani umefurahi nisamehe kwakukulaumu ni Uchungu na maumivu makali. YESU ASANTE KWA KUNIPA BABY BOY TENA,Kwakua Maisha yangu na hii Baraka imekuja kama majibu ya maombi yangu basi ataitwa (TESTMONY ) na JINA LINGINE LA MUSLIM NASUBIR NTASEMA” Baadhi ya maneno aliyoandika Munalove.

Muna Love amejifungua mtoto wa kiume baada ya kupitia maumivu ya muda mrefu kufuatia kumpoteza mtoto wake wa kwanza wa kiume Patrick aliyefariki Julai 3 mwaka 2018.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *