Polisi watoa tamko tukio la ukatili la binti Yombo

Jeshi la Polisi limetangaza kuanza kulifanyia kazi tukio hilo ovu na la kulaaniwa lililosambazwa kwenye mitandao ya kijamii likimwonyesha binti anayesemekana ametokea Yombo Dovya Jiji la Dar es Salaam akidhalilishwa na kufanyiwa ukatili ambao haukubaliki kwani ni kinyume cha sheria, maadili ya Mtanzania na Haki za Binadamu.

Taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi Dodoma DCP David A. Misime imeeleza kuwa Jeshi la Polisi hilo linatoa wito kwa Wananchi wote waache kuendelea kusambaza video hiyo kwani kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria lakini pia ni kitendo cha kuendelea kudhalilisha utu wa binadamu mwenzetu.

“Tunatoa wito kwa mwenye taarifa ya kuhakikisha mkono wa sheria unawafikia kwa haraka waliofanya ukatili huu asisite kutusaidia kwa kutupa taarifa au kumpatia kiongozi yeyote yule wanayemwamini kwamba taarifa ikimfikia watu hao watapatikana haraka iwezekanavyo au toa taarifa kupitia namba hii 0699 99 88 99.” imesema taarifa ya Polisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *