Rais Joe Biden Akutwa Na Virusi Vya COVID-19

biden

Rais wa Marekani, Joe Biden amegundulika kuwa na UVIKO-19. hivyo kulazimika kukatiza mkutano wa kampeni wa kutafutwa uungwaji mkono kwa wapiga kura wa Latino.

Biden mwenye umri wa miaka 81 alibainika kuwa na dalili za ugonjwa huo jana na tayari ameanza matibabu kwa mujibu wa daktari wake akizungumza na tovuti ya BBC.

Hata hivyo, Biden kabla ya kuanza matibabu hayo ambapo pia itamlazimu kujitenga, aliwaambia waandishi wa habari kuwa anajisikia vizuri, japokuwa baadaye alipelekwa katika makazi yake yaliyopo Delaware.

Rais Biden atajitenga Delaware kulingana na mwongozo wa vituo vya Marekani vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *