Rais mstaafu mwenye miaka 84 kurejea tena madarakani.

Rais mstaafu wa Malawi Peter Mutharika ameidhinishwa na Chama chake kugombea tena Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Nchi hiyo utakaofanyika mwaka 2025 ikiwa ni miaka mitano tu imepita tangu aliposhindwa kutetea nafasi yake na kutupwa chini kwenye Uchaguzi na Rais Lazarus Chakwera.

Mutharika mwenye umri wa miaka 84 alikuwa rais wa nchi hiyo kuanzia mwaka 2014 hadi 2020 alisema kuwa amekubali uteuzi huo kutoka kwa Chama chake na kwamba yeye na chama chake watarekebisha uchumi ambao ukuaji wake umekuwa si mzuri na umekumbwa na uhaba wa fedha za kigeni .

Uchaguzi mkuu wa Malawi umepangwa kufanyika Septemba 16, 2025 na Mutharika atakabiliana na Rais wa sasa Lazarus Chakwera wa chama cha Malawi Congress ambaye atakuwa akiwania muhula wa pili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *