Rais Samia ahudhuria uapisho wa Kagame Rwanda

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameondoka leo nchini kwenda Rwanda kushiriki sherehe za uapisho wa Rais Mteule wa nchi hiyo, Paul Kagame.

Taarifa ya Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Sharifa Nyanga ilisema jana kuwa Kagame ambaye alichaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo Julai 2024, anaapishwa leo.

Katika uchaguzi uliofanyika Julai 15, Kagame alipata asilimia 99.15 ya kura zote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *