Klabu ya Simba imeweka rekodi ya kumaliza tiketi zote za sikukuu ya Simba Day siku tatu kabla ya sherehe yao itakayofanyika jumamosi ya terehe 3/8/2024 katika dimba la Benjamini Mkapa.
Mnyama anaweka rekodi hii akiivunja rekodi aliyokuwa ameiweka msimu uliopita ya kujaza uwanja huo unaoingiza mashabiki elfu 60 siku mbili kabla ya Simba Day.
Akizungumzia kufikia tamati kwa uuzaji wa tiketi Afisa Mtendaji Mkuu, Imani Kajula amesema, ” Simba tumeonyesha ukubwa wetu na tumeweza kuvunja rekodi yetu ya mwaka jana ambapo tuliuza tiketi zote siku mbili kabla ya Simba Day, mwaka huu tumeuza tiketi zote – SOLD OUT siku tatu kabla ya Simba Day.”
“Hongereni sana mashabiki wetu na tukutane uwanja wa mkapa kwenye Simba Day ya Ubaya Ubwela. Timu yeyote kubwa inapimwa na ukubwa wa sapoti ya mashabiki wake, na hii inadhihirisha kwanini mashabiki wa Simba mlichaguliwa kuwa mashabiki bora barani Afrika.”
Mashabiki wa Simba wanakuambia wao kazi yao ni kula, kulala na kuishabikia timu yao.