Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo July 30, 2024
Pitia kurasa za mbele za magazeti ya Tanzania kitaifa na kurasa za kimichezo pamoja na gazeti la Michezo ya leo July 30, 2024 na ujipatie nakala yako kwa undani wa habari.
Pitia kurasa za mbele za magazeti ya Tanzania kitaifa na kurasa za kimichezo pamoja na gazeti la Michezo ya leo July 30, 2024 na ujipatie nakala yako kwa undani wa habari.
Mtalii mmoja amefariki na wengine 6 kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea jana Julai 28, 2024 saa 10 jioni katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa) leo Julai 29, 2024 gari hiyo ilikuwa na watalii 7 wenye asili ya China na dereva raia…
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM, Abdulrahman Kinana, ambaye amemwandikia barua ya kuomba kupumzika. Katika majibu yake Mwenyekiti wa CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema “Ni kweli nilipokuomba utusaidie kwa nafasi ya Makamu Mwenyekiti nilikuahidi utakaa muda…
Nahodha wa timu ya Taifa Wanawake Tanzania Opah Clement amejiunga na kuanza kuitumikia rasmi klabu yake mpya ya Henan Jianye FC ya ligi kuu wanawake nchini China akitokea klabu ya Besitkas ya ligi kuu Uturuki. Opah siku moja tu baada ya kutambulishwa alicheza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu nchini humo huku timu yake…
Klabu ya Simba imeshinda magoli 2-1 dhidi ya klabu ya Al Adalah ya ligi daraja la kwanza nchini Saudi Arabia kwenye mchezo wa tatu wa maandalizi ya msimu (Pre Season) uliochezwa kwenye dimba la Suez Canal nchini Misri. Kwenye mchezo huo magoli ya Simba yamefungwa na wachezaji wapya Steven Mukwala dakika ya 9 na Joshua…
Nyota wa muziki wa AfroBeat kutoka Nigeria, Burna Boy, ameanguka wakati akitumbuiza jukwaani. Tukio hilo lilitokea wakati akiwa kwenye tamasha la kumbukumbu ya albamu yake ya tatu ya (African Giant). Akiwa amepandwa na mzuka msanii huyo aliruka kutoka stejini na kukanyaga spika akijaribu kuelekea kwa mashabiki na ndipo alipopiga mweleka na kuanguka chini…
Israel imemuonya Rais Erdogan wa Uturuki kwamba hatima yake itaishia kuwa kama ya Saddam Hussein, hii ni baada Rais huyo wa Uturuki kutishia kuwa nchi yake inaweza kuivamia Israel na kutuma vikosi vyake kwenye maeneo ya Palestina yanayokaliwa kimabavu na Israel. “Lazima tuwe thabiti ili Israeli isiweze kufanya mambo haya kwa Palestina,” alisema Erdogan, akimaanisha…
Klabu ya Azam leo usiku itahitimisha kambi ya maandalizi ya msimu iliyoweka kwa wiki kadhaa huko Benslimane Morocco kwa mchezo mkubwa wa kirafiki dhidi ya Wydad AC ambayo ni moja ya klabu kubwa nchini humo na barani Afrika kwa ujumla. Mchezo huo dhidi ya Wydad ambao wanafundishwa na aliyekuwa kocha wa Mamelodi Sundwons Rulani…