Wamarekani wapinga kuhusika na maandamano Kenya.

Maandamano kenya

Shirika la Marekani la Ford Foundation limekanusha madai ya Rais William Ruto kwamba linafadhili maandamano ya kupinga serikali yanayoendelea kwa wiki kadhaa nchini humo huku makumi ya raia wakipoteza maisha.

Hii ni baada ya Rais William Ruto kuishutumu taasisi hiyo wakati akiwa katika hafla moja katika mji wa Nakuru kuwa inafadhili maandamano hayo na kulitaja shirika hilo moja kwa moja kuhusika na shutuma huyo.

Katika taarifa walioitoa Shirika hilo la Ford Foundation limesema, “Ingawa tunatambua haki ya Wakenya kutetea kwa amani nchi yenye haki na usawa, tunakanusha vitendo au matamshi yoyote ambayo yana chuki au kuunga mkono unyanyasaji dhidi ya taasisi yoyote, mtu binafsi au jamii yoyote. Hatukufadhili maandamano ya hivi majuzi dhidi ya mswada wa fedha na tuna sera isiyopendelea upande wowote kwa utoaji wetu wote wa ruzuku.”

Shirika hilo lenye makao yake makuu katika mji wa Nairobi lilianzishwa mwaka wa 1936 na Edsel Ford, mwana wa mwanzilishi wa Ford Motor Company Henry Ford, linafanya kazi kote ulimwenguni likilenga kuendeleza haki ya kijamii na kukuza maadili ya kidemokrasia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *