Wanaonunua malori kutoka Uingereza wapewa tahadhari

Kupitia chapisho lake kwenye ukurasa wa X, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mbelwa Kairuki ametoa tahadhari kwa wafanyabiashara wenye nia ya kununua malori yaliyotumika kutoka Uingereza wachukue tahadhari za msingi wanapofanya manunuzi ili kuepuka usumbufu na hasara inayoweza kutokea.

Balozi Kairuki amewataka wanunuzi hao kuhakikisha kuwa kampuni wanazotaka kufanya nazo biashara zimesajiliwa nchini Uingereza, na kwamba uhakiki huo ufanyike kupitia serikali ya Uingereza kwani hakuna malipo yoyote katika kufanya uhakiki huo.

“Ni vyema kuingia mkataba wa manunuzi na kampuni inayokuuzia lori. Wapo watanzania wanadiaspora wenye Ofisi za sheria hapa nchini Uingereza ambao wanaweza kutoa huduma ya kuandaa mkataba na hata pale inapojitokeza changamoto zozote kuwa wepesi kwa wao kufuatilia,” ameshauri mwanadiplomasia huyo.

Pia amewataka wanunuzi hao kufanya upekuzi wa kufahamu historia ya malori wanayotaka kununua kabla ya kufanya malipo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *