“Wasanii Rudisheni Mikopo” – Mh Hamis Mwinjuma

Naibu Waziri wa Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma mwanafa Ametoa agizo kwa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania Ukutane na wasanii walionufaika na mkopo wa fedha kupitia mfuko huo na mpaka sasa hawajarejesha.

Hil linajiri kabla ya kuandishwa kwa utaratibu mpya wa kutumia Akaunti za Benki kukopesha wasanii ukiwa ni mpango wa kuhakikisha wanufaika wote wa mkopo wanarudisha mkopo huo huku akisisitiza kua hakuna mkopo utakaofutwa.

“Kila fedha iliyotolewa na Mhe. Rais kwa ajili ya kukopesha wasanii lazima irudi, mtu yeyote, aliyekopeshwa fedha anatakiwa kurejesha ili wasanii wengine wanufaike, tutakachofanya ni kuangalia utaratibu rahisi utakaowezesha baadhi ya walioshindwa kurejesha kwa wakati warejeshe”

“Namuagiza Mtendaji Mkuu wa mfuko akae nanyi, naomba mtoe ushirikiano, muangalie namna ambayo itawawezesha kurejesha mikopo yenu, mathalani kupunguza kiwango cha marejesho hii yote ni kuhakikisha fedha yote inarejeshwa” amesisitiza Mhe. Mwinjuma.

Agizo limetolewa na Mhe. Mwinjuma Julai 23 2024 Jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na wanufaika wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa ambapo pia ameelekeza itafutwe namna bora ambayo itasaidia mikopo yote kurejeshwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *