Mchezaji apoteza maisha baaada ya kuanguka uwanjani.

Mchezaji wa timu ya Club National de Football Juan Izquierdo mwenye umri wa miaka 27 raia wa Uruguay amefariki dunia siku ya jana akipatiwa matibabu baada ya kuanguka uwanjani kwenye mchezo wa Copa libertadores dhidi ya Sao Paolo ya Brazil siku ya Alhamisi ya agosti 22 ambapo mchezo uliomalizika kwa klabu yake kupoteza kwa goli 2-0.

Mchezaji huyo ambaye aliyekuwa anacheza nafasi ya beki wa kati alianguka uwanjani dakika ya 84 kwenye mchezo huo bila kusukumwa wala kuguswa na mchezaji mwingine na kupata mshtuko wa moyo na kuanza kupatiwa matibabu uwanjani kabla ya kufikishwa kwenye hospitali aliyotibiwa mpaka wakati anafariki.

Juan alikuwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Albert Einstein iliyopo nchini Brazil na siku tano nyuma hali yake ilikuwa inaendelea vizuri kabla ya siku ya jana ambapo hali yake ilibadilika ghafla na kupelekea umauti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *