Waandamanaji wavamia gereza na kuwaachilia mamia ya wafungwa

Waandamanaji nchini Bangladesh wamevamia gereza siku ya Ijumaa na kuwaachilia “mamia” ya wafungwa kabla ya kulichoma moto gereza hilo, afisa wa polisi ameliambia shirika la habari la AFP.

 

“Wafungwa wametoroka gereza na waandamanaji wamechoma moto gereza”, afisa wa polisi amesema, akizungumza kwa sharti la kutotajwa. “Sijui idadi ya wafungwa waliotoroka lakini itakuwa mamia,” ameongeza.

 

Mkazi wa eneo hilo ameliambia shirika la habari la AFP kwamba ameona watu wakitoka gerezani wakiwa wamebeba vifaa vyao kwenye mifuko.

 

Bangladeshi imetikiswa tangu Julai 1 na vuguvugu la maandamano ya wanafunzi kudai mageuzi ya ajira katika utumishi wa umma kutokana na ukosefu mkubwa wa ajira kwa wahitimu wa vyuo vikuu katika nchi hii yenye wakaazi milioni 170.

 

Wanashutumu mfumo wa sasa wa ajira unaowapendelea wale walio karibu na mamlaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *