Utaishia kama Saddam, Israel yamtisha Rais wa Uturuki

Israel imemuonya Rais Erdogan wa Uturuki kwamba hatima yake itaishia kuwa kama ya Saddam Hussein, hii ni baada Rais huyo wa Uturuki kutishia kuwa nchi yake inaweza kuivamia Israel na kutuma vikosi vyake kwenye maeneo ya Palestina yanayokaliwa kimabavu na Israel.

“Lazima tuwe thabiti ili Israeli isiweze kufanya mambo haya kwa Palestina,” alisema Erdogan, akimaanisha mauaji ya kimbari yanayoendelea huko Gaza.

“Kama tulivyoingia Nagorno-Karabakh na tulivyoingia Libya, tunaweza kuwafanyia vivyo hivyo Israel. Hakuna kitu ambacho hatuwezi kufanya.”

Mara tu baada ya kauli hiyo ya Erdogan, Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, kupitia ukurasa wake wa X alimuonya rais huyo wa Uturuki kwamba akijaribu kufanya hicho anachofikiri basi yatamkuta kama yaliyomkuta Rais wa zamani wa Iraq, Saddam Hussein

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *