Mmiliki wa mabasi ya Sauli afariki kwa ajali ya gari

Mmiliki wa mabasi ya Sauli, Solomon Sauli Mwalabila amefariki dunia alfajiri ya leo Agosti 4, 2024 katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Miwaleni, Wilaya ya Mlandizi mkoani Pwani.

Taarifa zinaeleza kuwa gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T213 DQD lilipata hitilafu ya kiufundi na kuligonga gari aina ya Jeep alilokuwemo tajiri huyo lenye namba za usajili T466 EGW kisha kuligonga gari jingine aina ya Howo la kubebea kokoto.

Kamanda wa Polisi Mkoa Pwani Pius Lutumo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye chumba cha maiti kituo cha afya Mlandizi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *