Aliyebadili jinsia aokotwa kando ya barabara akiwa amefariki

Polisi nchini Nigeria wanachunguza kifo cha staa wa TikTok aliyebadili jinsia na kuwa mwanamke anayejulikana kwa jina la “Abuja Area Mama”.

BBC imeripoti kuwa mwili wake uliokuwa na majeraha ulikutwa kando ya barabara mjini Abuja, siku ya Alhamisi.

Abuja Area Mama alikuwa na wafuasi wengi kwenye mitandao ya kijamii, na hakuwahi kutumia jina lake halisi.

Katika chapisho lake la mwisho kwenye mtandao wa Instagram siku ya Jumatano, Abuja Area Mama alisema alikuwa akijiandaa kumtembelea mpenzi wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *