Azam tumelitia aibu Taifa – Ibwe

Baada ya kipigo cha 2-0 kutoka kwa klabu ya APR ya Rwanda na kuondosha kwenye hatua ya awali ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika, Afisa habari wa wa klabu ya Azam Hashim Ibwe kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii amesema wazi kuwa wametia aibu taifa na wadau wote wa michezo nchini.

 

Anaandika Ibwe kupitia Instagram
_______

Tumewaangusha Mashabiki wetu ,Tumewaangusha Watanzania wote tumekuwa Aibu kwenye Taifa la watu mbele ya Team ambayo tunaiweza ,mbele ya Team ambayo tungeweza pata ushindi nyumbani na ugenini.
Hatujacheza vizuri hata kidogo mechi zote mbili kuna wakati lazima ukweli mchungu useme tumefedheheka mno.
.
Team yetu sio mbaya ina ubora wa hali ya juu lakini tumeondoshwa ugenini ,
.
Siombi Msamaha leo wala sitetei WE NEED CHANGES ,WE NEED TO CHANGE.
_____

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *