Kocha wa Timu ya Taifa ya England Atangaza Kujiuzulu

Mkufunzi Gareth Southgate ametangaza kujiuzulu nafasi yake kama kocha wa timu ya taifa ya England ikiwa ni siku mbili baada ya kushindwa kuiongoza England kutwaa ubingwa wa EURO 2024 dhidi ya Uhispania kwenye fainali.

Southgate (53) raia wa England ameiongoza England kwenye mechi 102 kwa miaka 8 ya uhudumu wake kwenye nafasi hiyo lakini hakufanikiwa kuipatia England taji lolote licha ya kufika fainali mara mbili.

Southgate aliteuliwa kuwa kocha wa England mnamo 2016 na kuiongoza England kufika nusu fainali yake ya kwanza ya kombe la Dunia mnamo 2018 baada ya miaka 28 kabla ya kuiongoza England kufika fainali yake ya kwanza kwenye michuano mikubwa kwenye EURO 2020 tangu 1966.

Kwenye EURO 2024 alifanikiwa kuipeleka England fainali lakini ilipoteza kwa kipigo cha 2-1 dhidi ya Uhispania na kuifanya timu hiyo kuendelea kusubiri taji la kwanza tangu 1966 walipotwaa kombe la Dunia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *