Mchezaji apewa kipigo kisa kuvaa jezi ya Bayern Ujerumani

Jeshi la Polisi Nchini Ujerumani linafanya uchunguzi juu ya shambulio dhidi ya mchezaji wa Nurnberg, Niklas Wilson Sommer baada ya beki huyo wa kulia kuchapisha picha yake akiwa amevaa jezi ya Bayern Munich kwenye akaunti yake ya Instagram.

Sommer, ambaye alijunga na Nurnberg kutoka Waldhof Mannheim ya Ujerumani mnamo 2023, ameripotiwa kushambuliwa akiwa nyumbani kwake kwa kile kinachoonekana kuwa hisia kutoka kwa mashabiki wa Nurnberg kuwa picha yake akiwa amevalia jezi ya Bayern Munich ambao ni mahasimu wao wa ‘kutupwa’.

Hata hivyo kupitia taarifa yake kwenye tovuti yao, klabu ya Nurnberg imelaani shambulio hilo wakitaja tukio hilo kuwa haliendani kabisa na maadili ya maadili ya klabu hiyo huku uchunguzi wa Polisi ukiendelea.

Wafuasi wa Nurnberg walitoa hasira zao kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kwenye mchezo wa Jumamosi wa nyumbani dhidi ya Magdeburg huku mashabiki wakiinua mabango ya kuonesha kukerwa na hatua hiyo ya Sommer kuvaa jezi ya Bayern Munich.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *