Robertinho arejea Rayon Sports ya Rwanda

Klabu ya Rayon Sports ya ligi kuu Rwanda imethibitisha rasmi urejeo wa aliyekuwa kocha wa klabu hiyo na klabu ya Simba ya Tanzania Roberto Oliviera ‘Robertinho’ raia wa Brazil kuwa kocha wao mkuu.

Rayon Sports wamemtambulisha nyota huyo wa zamani wa vilabu vya Flamengo, Fluminense na Atleico Mineiro za Brazl pamoja na timu ya taifa ya nchi hiyo leo jioni na ataifundisha klabu hiyo kwenye michuano ya CAF.

Robertinho mwenye umri wa miaka 64 aliwahi kuhudumu Vipers SC ya Uganda, Simba ya Tanzania na Rayon Sports ambapo amerejea kwa mara nyingine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *