SIMBA YAANZA KIBABE KUKUSANYA TUZO ZA LIGI

Nyota wa Simba SC , Jean Charles Ahoua raia wa Ivory Coast ametangazwa kuwa mchezaji bora wa NBC Premier League mwezi Agosti.

Nyota huyo ametoa assist 3 na kufunga goli 1 ambapo akiisaidia timu hiyo kupata ushindi kwenye michezo miwili ya NBC Premier League dhidi ya Tabora United (3-0) na dhidi ya Fountain Gates (4-0).

Kwa upande mwingine kocha Mkuu wa Simba SC Fadlu Davids ametwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi kwenye NBC Premier League.

Fadlu Davids amewashinda Patrick Aussems wa Singida Black Stars na Abdallah Mohamed wa Mashujaa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *