Ligi Kuu Msimu Wa 2024/2025, Kuanza Agosti 16
Bodi ya Ligi leo wamesema kuwa msimu wa 2024/2025 utaanza Agosti 16, 2024
Bodi ya Ligi leo wamesema kuwa msimu wa 2024/2025 utaanza Agosti 16, 2024
Tajiri namba moja barani Asia kutoka Nchini India Mukesh Ambani ambaye hivi karibuni alitikisa Duniani kutokana na harusi kubwa na ya kifahari ya kijana wake Anant Ambani iliyohudhuriwa na mabilionea duniani kote kuzua gumzo,imefahamika kuwa kabla ya harusi hiyo ya kijana wake iliyogharimu zaidi ya Trilioni 1.9 aligharamia pia harusi za wachumba 50 ambao hakuwa…
Ulikuwa wakati wa kusisimua kwa mwimbaji wa Nigeria, Oyinkansola Aderibigbe, almaarufu Ayra Starr, alipokutana na mwigizaji wa Marekani, Will Smith. Ayra alikutana na Smith jana usiku baada ya tamasha la Coldplay huko Roma, ambapo kupitia ukurasa wake wa X zamani Twitter ameandika “What a Night! Ayra Stsrr x Will Smith” akaweka na vi emoj vya…
Uongozi wa Simba SC umetangaza kuachana na mshambuliaji wao Pa Omar Jobe baada ya nyota huyo kudumu kwa muda wa miezi sita. Inaelezwa kuwa viongozi hawakuridhishwa na kiwango cha nyota huyo na hivyo wakafikia maamuzi hayo.
“Nina furaha, nina furaha sana, nahisi ajabu kuwa hapa. Nimelala miaka mingi nikiiota Real Madrid na sasa… ni ukweli.” “Ndoto yangu nyingine sasa ni kuwa katika kiwango cha klabu bora zaidi duniani. Nitatoa maisha yangu kwa klabu hii.” Tumeshinda jamani.” Kylian Mbappé mchezaji mpya wa Real Madrid
Inawezekana wengi wetu tunajitazama kwenye mafanikio pale tunapo miliki nyumba zenye hadhi na muonekano mzuri. Hii imekuwa tofauti kwa Tajiri namba moja barani Afrika, Aliko Dangote ambaye amewashangaza wengi na kuzua mijadala katika vijiwe vya kidijitali baada ya kusema hana nyumba nchi nyingine yoyote zaidi ya Nigeria. “Sababu ya kutokuwa na nyumba London au Marekani…
Aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump amehudhuria mkutano wa chama chake cha Republican akiwa na bandeji sikioni na kukaribishwa kwa shangwe na wafuasi wa chama chake. Hii ni mara ya kwanza kwa mgombea huyu wa Urais kuonekana kwenye hafla kubwa ya umma tangu kutokea kwa jaribio la mauaji dhidi yake siku ya Jumamosi. Baada ya…
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam inatarajia kutumia Sh bilioni 10.7 za mapato ya ndani kujenga zaidi ya kilomita 6 za barabara kwa kiwango cha lami na zege. Zabuni za ujenzi wa barabara hizo zilitangazwa katika mwaka wa fedha 2023/2024 na Julai 15,2024 jiji hilo limesaini mikataba na wakandarasi waliopewa kazi hizo. Akizungumza wakati…