Vijana kukopeshwa migahawa inayotembea ili kujikwamua kuchumi

Bodi ya Kahawa imezindua mradi wa mgahawa unaotembea maeneo mbalimbali yenye mikusanyiko ya watu ili kuweza kutoa huduma ya unywaji wa kahawa.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonesho ya wakulima na wafugaji (88) yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya 88 Nzuguni jijini Dodoma Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Kahawa Primus Kimaryo amesema mkakati wao ni kuongeza unywaji wa kahawa kutoka asilimia 7-8 ambao ni unywaji wa sasa ,kwenda ailimia 15.

Amesema wamebuni mradi huo unaotembea ili kuwawezesha vijana kujipatia kipato kupitia zao la kahawa.
Kimaryo amesema mradi huo unawalenga vijana ambapo watapata mkopo nafuu na baada ya miaka mitatu mhusika anapaswa kurejesha gharama hizo za mkopo na mgahawa unakuwa ni mali yake.

Amesema vijana mbalimbali wameshaonesha nia ya kutaka kuwa na mgahawa huo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo msukumo mkubwa ni kuona namna gani vijana wanaweza kupata ajira kupitia zao la kahawa kwani kijana kupata ardhi au kukodisha mgahawa ni changamoto.

Aidha amesema,mpaka hivi sasa gharama za mkopo huo ni shilingi milioni 30 huku akisema wanaanza kwa kutengeneza migahawa 100 kwanza ambayo pia itatengenezwa kwa awamu.

Amesema kabla kupata mradi huo vijana wote wataokidhi vigezo vya kupata mkopo huo ŵatapatiwa mafunzo ya uendeshaji wa migahawa hiyo ili iweze kuleta tija iliyokusudiwa.
TM

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *