‘Waliotumwa na Afande’ waifikia siku ya tano Mahakamani

Kesi ya ubakaji na kumwingilia kinyume cha maumbile binti mmoja mkazi wa Yombo Dovya jijini Dar es Salaam, imeingia katika siku ya tano ambapo Washtakiwa wamefikishwa Mahakamani hii leo Agosti 23, 2024 kusikiliza shauri hilo.

Kesi hiyo inaendeshwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi jijini Dodoma, ambako awali  walisomewa mashtaka mawili na Hakimu Mkazi Mkuu, Zabibu Mpangule anayesikiliza kesi hiyo.

Kwa mara ya kwanza Watuhumiwa hao walifikishwa Mahakanani hapo Agosti 19, 2024 na kusomewa mashtaka waliyoyakana ya kumbaka na kumwingilia kinyume cha maumbile binti huyo.

Washtakiwa wa kesi hiyo ni MT 140105 Clinton Damas maarufu kama Nyundo, C.1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson ‘Machuche’ na Amin Lema anayejulikana pia kwa jina la Kindamba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *