Binti Mfalme wa Dubai Ampa Talaka Tatu Mumewe Kupitia Instagram

Binti mfalme atoa talaka

Binti wa mtawala wa Dubai Sheikha Mahra Bint Mohammed Bin Rashid Al Maktoum ameonekana kustaajabisha wengi baada ya kutangaza kumtaliki mumewe Mohammed Bin Rashid bin Mana Al Maktoum, kupitia ujumbe wa talaka tatu aliouandika kwenye Instagram.

Ameandika “Mpendwa Mume wangu, kwa kuwa unashughulika na wenza wengine, ninatangaza talaka yetu. Ninakupa talaka, ninakupa talaka, na ninakupa talaka. Kila la kheri. Mke wako wa zamani,”

Hili limejiri ikiwa ni mwaka mmoja pekee umepita tangu wawili hao walipofunga ndoa, na ikiwa pia ni miezi miwili pekee tangu walipofanikiwa kupata mtoto wao wa kwanza.

Talaka tatu sio chaguo kwa wanawake chini ya sheria ya Kiislamu, ambayo inasema kwamba wanawake wanaweza tu kutafuta talaka kwa upande mmoja kupitia mchakato unaoitwa “khula”.

Hilo lahusisha mwanamke aliyeolewa kuwasilisha ombi rasmi kwa mahakama na kutaja sababu halali ya kuanzisha kesi ya talaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *