Rema atoa shukrani ya kibunda cha milioni 180 kwa Kanisa

Mwanamuziki wa Nigeria, Divine Ikubor, maarufu kwa jina la Rema, ametoa kiasi cha Naira milioni 105 (sawa na shilingi Milioni 180 za kitanzania) kwa Kanisa la Christ Embassy, lililoko kwenye jimbo la Edo mahali alikozaliwa.

Rema alitoa msaada huo kama shukrani kwa msaada ambao kanisa hilo lilitoa kwa familia yake ilipokuwa ikipitia kipindi kigumu wakati yeye akiwa mdogo.

Inaelezwa kuwa wakati famlia ya Rema inapitia kipindi kigumu kanisa hilo lilimfungulia duka mama yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *